Here are the FeedBlitz email updates for you

Kutoa mchango wako, tembelea tovuti yetu www.JamiiForums.comJamiiForums | The Home of Great Thinkers - 12 new articles

man juuuuuuuuuuuuuuuuuu

vijana wa ars mmeamua kufugwa goli za mechi nne haya bana
 


Anaomba tuachane na sio kutengana!

Jamani mwenzenu najiona wazi naelekea kumkosa yule niliyempenda kwa dhati ya moyo wangu kwa sababu kadhaa ambazo hazikuwa na uhalisia kama anavyodai mwenza wangu! Kiukweli nlibaini kuwa mwenzangu ana moyo dhaifu sana kwani hata akisikia jambo la utani hunikasirikia na hata kuomba kuachana, basi nkisuruhisha anajirudi na tunaendelea tena. Kali na mpya zaidi ni baada ya kunichunia kwa siku 3 ghafla, sababu eti kuna mtu alimtumia ujumbbe mfupi wa maandishi uliosomeka "wewe usipende kugombana na wanawake wenzio, huyo unaemwita mpenzi wako hajatulia, habari ndiyo hiyo" Hapo ndio ulikua mwisho na kunambia kwanza keshampata mwingine hataki kuwa nami kwan kalichoka penzi langu lililojaa mateso na kumpa pressure kila siku, na pia hajali kitendo cha kuwafahamisha wazazi wetu juu ya uhusiano tulokua nao toka 2009, na binafsi toka nimemjuza mother ni wiki sasa inakaribia kupita so najiuluza nitatengua vp taarifa hizi kwa mother za kutengana na mtu mwenyewe ndio kasema nisimpigie tena simu kujadili mapenzi labda ishu nyingine.
How can I do friends, kwan migogoro mingi nimepanchi kwa kumthibitishia uhalisia wa aliyoyasikia na jinsi yalivyo na kwa sasa ndio hataki hata kunisikiliza kujitetea. NAMPENDA KIUKWELI LAKINI ANANITESA ZAIDI YA SANA JAMANI.
 Uchaguzi wa Igunga

Naomba mchangie kwa hili, kwann CHADEMA,CCM na CUF wanataka kutumia helcopter kwenye kampeni ni jimbo dogo na linaweza kufikika kirahisi
 


nipo ndani sasa

wandugu kwema nimeamua kujitosa ndani ya jf nina furaha sana
 


Hoja zisizo na mwelekeo wa maendeleo

Kama watanzania wenye upeo na mtazamo chanya tuna haki na wajibu wa kuwapuuza hawa wanaoandaa na kutetea hoja za kibaguzi/chuki zenye muelekeo wa kugawa nchi ikiwa ni kidini ama kimakabila.Hawa ni wenye fikra potofu,wavivu, mawazo yao yametawaliwa na tamaa za kuhodhi na kumiliki mali/madaraka makubwa pasipo kujishughulisha.
Mungu Ibariki Tanzania
 


Hotuba ya Rais ya Kikwete kwenye baraza la Idd-Mawazo yangu

Nimesoma kwenye magazeti na kusikiliza kwenye vyombo vya habari. Kwa kweli wengi wamemsifia kwamba ametoa hotuba nzuri. Lakini mimi kwa kweli nimekuwa na mtazamo tofauti. Naomba niseme wazi kwamba Raisi Kikwete amekuwa mean with the truth kwenye hii hotuba yake. Kwanza kwenye suala la Mahakama ya Kadhi, ni yeye na CCM yake ambao waliwaahidi waislamu mwaka 2005 kuwa watalipatia ufumbuzi. Sasa kwa waislamu wengi ufumbuzi ilikuwa serikali itaanzisha hiyo Mahakama. Lakini cha ajabu nadhani mwaka 2008, Kikwete huyo huyo mbele ya Maaskofu wa KKKT alikanusha kuhusika na suala la mahakama ya kadhi. Akasema lilianzishwa na Mrema na Sheikh Ramia. Kwa maana nyingine yeye asiulizwe. Leo anasema kuwa ni suala la waislamu wenyewe lakini hapo hapo anakiri kuwa Waziri Mkuu anaratibu. Waziri Mkuu ataratibu vipi suala la ibada. Kwangu mimi nadhani Kikwete angekiri walipoteleza na kueleza kuwa walifanya makosa kuingiza suala la dini kwenye siasa.

Suala la pili ni kuhusu suala la MOU ambapo waislamu wamelalamika kuwa wakristo wanapewa fursa zaidi. Kikwete amesema kwa sababu wao hawaombi. Hapa kwa kweli panatia shaka. Kikwete kama mara mbili akiwa kwenye mikutano na viongozi wakristo alinukuliwa akitoa takwimu kuonyesha pesa ambazo taasisi za kikristo wamepata kutoka serikalini. Hivi alishindwa nini kutoa takwimu kuonyesha ni kiasi gani taasisi za kiislamu zinapokea kutoa serikalini? Kwa nini hakutoa hata mfano kuwa Muslim University kilitolewa na serikali? Je pia alishindwa kuonyesha kuwa hizo shule za makanisa kama zinazuia kusoma watu wa dini nyingine? Na pia kwa sababu alikuwa Waziri wakati Mzee Mwinyi atakuwa anajua kwanini MOU ilisainiwa, je alishindwa nini kutoa hiyo institutional memory ili kuondoa upotoshaji unaoendelea. Alichozalisha hapa ni kuonyesha kuwa wakristu wamekuwa wakipendelewa kwa sababu wanaomba na waislamu wamenyimwa kwa sababu hawaombi kitu ambacho nadhani si sahihi. Kama kwenye wamenyimwa serikali haitakiwi kusubiri hadi kuombwa, kwani Nyerere aliombwa na nani kutaifisha shule?

Kwa kweli kwangu nadhani ni hotuba inayopalilia udini badala ya kuumaliza. NAWAKILISHA
 


Cheka na maugo imekuwaje?

Wazee matokeo ya gemu ya cheka vs maugo imekuwaje??
 


Black Libyans & Sub-Saharan Africans Are Being Targeted by Rebel Fighters

Black Libyans and sub-Saharan Africans are being targeted by rebel fighters who suspect them of backing Muammar Qaddafi, Amnesty International said.
Amnesty investigators this week visited the Central Tripoli Hospital and the capital’s morgue where they witnessed abuses, including men being dragged from hospital beds and detained, the London-based group said in a statement late yesterday. Some people are afraid to leave their homes, it said.
Sub-Saharan Africans risk reprisals from NATO-backed rebels because of allegations that Qaddafi used African mercenaries during the six-month conflict, Amnesty said. Many black Libyans are from the western town of Tawarga, which rebels associate with the shelling and siege of nearby Misrata by pro-Qaddafi forces, it said.
“The problem is black Libyans always were seen as outsiders, and this stems probably from how Qaddafi decided he would be an African leader of an African state and encouraged a large amount of African immigrants, some of whom served in his wars,” Shashank Joshi, an associate fellow at the Royal United Services Institute in London, said today in an interview.
Mustafa Abdel Jalil, head of the National Transitional Council, has urged opposition fighters not to seek revenge. In May, the council issued guidelines for its forces to act in accordance with international laws and standards. Mahmoud Shamman, a spokesman for the council in Dubai, didn’t answer calls seeking comment on the Amnesty statement.
‘Lofty Ideals’

“This reflects very badly on the NTC,” Joshi said of the Amnesty report. “They have said the right things, but their ability to enforce those lofty ideals on those with the guns in the streets is a lot more difficult.”
In visits to detention centers in Zawiya and Tripoli, Amnesty said it was told that between a third and a half of those detained were from Sub-Saharan Africa.
The rebels seem “to confuse black people with mercenaries,” African Union Commission Chairman Jean Ping told reporters in Addis Ababa, Ethiopia’s capital, on Aug. 29.
The council will need to “show sensitivity to these concerns” if the rebel forces attempt to take Sirte, Joshi said. Jalil yesterday gave Qaddafi supporters in his hometown until Sept. 3 to surrender or face attacks.
Hold Fighters Accountable

In the statement, Claudio Cordone, a senior director at Amnesty, called on the council to ensure its fighters are held accountable.
“Fighters engaging in abuses should be immediately removed from active duty, pending investigation,” he said.
During an Aug. 28 visit to a poor residential area of Tripoli, Amnesty investigators found a group of Eritreans who wouldn’t leave their homes because they feared being attacked, according to the report.
The following day, Amnesty said its investigators saw three rebels drag a black Libyan from his bed at the Central Tripoli Hospital and detain him. Two other black Libyans receiving treatment for gunshot wounds were told by anti-Qaddafi forces that “their turn was coming,” according to the report.
Amnesty said its workers examined that same day the body of an unidentified black man who was brought into the Tripoli Medical Center morgue by unknown men. While he bore no visible injuries, his feet and his torso were tied and blood was smudged around his mouth.
To contact the reporter on this story: Caroline Alexander in London at calexander1@bloomberg.net.
To contact the editor responsible for this story: Andrew J. Barden at barden@bloomberg.net.
 


msaada wana jf

wakubwa habari zenu naomba mnisaidie maana ya ABS na inafanya kazi gani katika gari. nawasilisha
 


JKT na Uzalendo; Uzalendo kwa Nani?

kuna mazungumzo mengi kuhusu kurejeshwa kwa mafunzo ya JKT na mara nyingi yamekuwa yakipigiwa debe na Television ya Chama Cha Mapinduzi kila uchao.

ukiwasikiliza watetezi wa hoja ya kurejea kwa JKT na wanapropaganda wengi wengine wanajenga hoja kwamba vijana wengi wamekosa uzalendo. kwamba vijana wengi si wabunifu tena na wanashinda vijiweni.

wana hoja. labda. ni kweli kwamba vijana wengi sasa wa vijijini na mijini wanashinda vijiweni. mbaya zaidi hata wale walio vijijini wanadanganyika kuwa neema iko mijini na matokeo yake wimbi kubwa la vijana kukimbilia mijini linazidi kuongezeka kila leo. lakini tusisahau kuwa kwa wale walioko vijijini wanayasikia maneno ya wakuu wa nchi...kwamba serikali haiwezi kuiamuru mvua inyeshe. kwa hiyo wale wenzangu na mimi walioko shamba wanaoamini katika kilimo imekula kwao. inabidi waje mijini. kwa hawa wa mijini na hasa waliopita skuli wao waliambiwa wataandaliwa ajira milioni moja. sijui ni wangapi hata sasa wana hizo ajira? nani atuthibitishie?

kinachonishangaza hapa ni hii dhana kwamba vijana wamekosa uzalendo. najiuliza kivipi? kwani uzalendo ni nini?

kwa mujibu wa kamusi yangu hapa, uzalendo ni ile tabia au hali ya mtu kuiunga mkono nchi yake kwa moyo na nguvu zake zote kiasi cha kuwa tayari kuitetea.

Maswali:
 1. wanaotuhumiwa kwa rushwa kubwa kubwa kama kagoda, dowans, na richmond? ni vijana? hawakupita jkt?
 2. wanaotuhumiwa kusafirisha wanyamapori kwenye ndege ni vijana? hawakupita jkt?
 3. wanaotuhumiwa kuuza dawa za kulevya leo ni vijana? hawakupita jkt?
 4. wanaolalamikiwa kuiingiza nchi katika mikataba mibovu ya madini ni vijana? hawakupita jkt?
kuna maswali mengi ya kujiuliza, lakini tuanze na hayo manne.

kwamba vijana sasa tunalaumiwa na hawa wazee waliopita jkt kwamba hatuna uzalendo, wakati wenyewe hawana hata harufu ya uzalendo.

why?

Nadhani ni siasa. Kwamba vijana tumechoka na kauli-mbiu za kila mwaka, miaka 50 baada ya uhuru bado tunaishi kwa kaulimbiu zisizokuwa na msaada kwetu.


Matokeo ya uchaguzi uliopita pia ni moja ya vichochezi vya suala hili kupigiwa debe. kwamba vijana wengi wameongoka kifikira. na kwa vitendo walikipinga waziwazi chama cha mapinduzi katika uchaguzi uliopita. na sasa ili kuwadhibiti vijana, ccm sasa wanakuja na mavi ya kale. ati JKT. kwamba wakawajaze vijana na fikra mgando za ccm.

Too late:

it will never work. kwa waliosoma physics wanajua Hooke's Law. Elastic material ikishavuka elasticity, basi inakuwa inaingia katika region tofauti kabisa inayoitwa deformation ambako huwa haiwezi tena kurejea katika original shape.

Vijana tumeshavuka Elastic Limit. Tuko kwenye Deformation point.

Kama motives za kurejea kwa JKT una lengo la kutujengea uzalendo kwa CCM....waanzilishi wa mpango huo mmefulia na hautafanikiwa. Kwa mara nyengine tena mmemshauri vibaya mkuu wa kaya.

Vinginenyo mtuambie............

kwa wizi huu, kwa rushwa hizi na hujuma hizi zinazofanywa na wazee walioko serikalini na waliopita JKT miaka hiyo, manataka kutufundisha uzalendo, nauliza hivi..........


Uzalendo kwa Nani?
 


Je ni kweli chumvi husababisha bp?, ipi nzuri ya unga au ya mawe?

Ukweli kuhusu chumvi na maajabu yake:


Stori kuhusu chumvi:
Tunapata chumvi nyingi kwenye vyakula vyetu siku hizi. Chumvi nyingi itasababisha shinikizo la damu, uvimbe, matatizo kwenye kibofu cha mkojo, matatizo ya moyo na orodha inaendelea.

Tunaambiwa chakula chenye chumvi kidogo au kisicho na chumvi kabisa ndicho bora kwa afya zetu.

Ukweli kuhusu chumvi:
Mpaka zama za pili za mawe (middle stone ages), hakuna chumvi iliyokuwa mbaya. Waharifu waliuliwa gerezani kwa kupewa chakula bila chumvi, iliwasababishia kifo cha taratibu.


Miaka 2000 iliyopita, chumvi ilitumika kama hela. Dhahabu na Chumvi vyote vilikuwa na thamani sawa. Neno 'salary' (mshahara) linatokana na neno 'salt' (chumvi).

Hapa kwetu Tanzania, watu hutumia msemo, 'Nimekula chumvi nyingi' kumaanisha kuishi miaka mingi.

Katika siku hizo za kale, chumvi ilitumika pia kuhifadhia vyakula. Siku hizi tunatumia rifrijereta, kwa hiyo chumvi chache inahitajiwa isipokuwa kwa matumizi machache ya kusokotea nyama.

Wanyama wote wenye damu moto, lazima wawe na chumvi ili kuishi. Ubongo wa binadamu pamoja na uti wa mgongo, vimo katika mfuko wa maji chumvi uitwao 'cerebrospinal fluid (csf)'. Umajimaji huu huzunguka sehemu zote za ubongo na uti wa mgongo.

Sote tulitumia miezi tisa kuishi katika mifuko ya uzazi ya mama zetu inayoelea kwenye maji chumvi (amniotic fluid).

Machozi yetu ni chumvi na tunatokwa na jasho ambalo pia ni chumvi. Mifupa yetu ina uwazi katikati yake (uboho) ambamo seli za damu hutengenezwa. Uboho huu umefunikwa na tabaka nyingi za chumvi kalisiamu kama vile kamba inavyoshikizwa pamoja. Kowa chumvi (salt crystals) zinashikizwa pamoja na kalisiamu, na kowa hizi ndizo zinazoifanya mifupa yetu kuwa imara, na siyo kalisiamu pekee.

Mifupa inamiliki asilimia 27 ya chumvi yote mwilini. Wakati mwili unahitaji chumvi zaidi, huikopa toka mifupani, jambo hili likitokea, kalisiamu huondolewa pamoja na chumvi na kuifanya mifupa kuwa miembamba, laini na midhaifu.

Chumvi imeundwa kwa Sodiamu na Klorini, kwa pamoja inaitwa; 'Sodiamu kloridi' (Na Ci).

Sodiamu ni metali laini yenye chaji chanya (+), wakati Klorini ni gesi yenye chaji hasi (-) ambayo hubadilika kuwa katika hali ya umajimaji inapoongezewa shinikizo.

Klorini ni gesi au umajimaji, lakini kwa namna fulani wakati dunia imeumbwa, klorini ilibadilika kuwa ngumu pamoja na sodiamu na madini mengine. Unaweza kuisaga chumvi na kuwa katika unga, klorini bado itabaki na sodiamu.

Klorini katika hali ya ugumuugumu, huitwa Kloridi.

Chumvi tutumiayo siku hizi inatoka katika bahari, maziwa, mito au katika migodi ya chumvi. Zaidi ya sodiamu na klorini, chumvi yote kwenye sayari yetu huja pamoja na madini mengine zaidi ya 80 ndani yake!.

Kwa hiyo tunaweza kuona ni jinsi gani madini hayo yalivyo na umhimu kwetu, la sivyo yasingeshikamanishwa na chumvi. Kwa sababu ya thamani yake kibiashara, madini hayo huondolewa ili kutengeneza faida kubwa.
Mwili wa binadamu una uwezo wa kuienguwa klorini kutoka katika sodiamu kadiri inavyohitajika. Damu yetu huihitaji klorini kama zifanyavyo ogani zingine ndani ya miili yetu.

Tumbo huitumia klorini kutengeneza haidrokloriki asidi inayohitajika ili kuuwezesha mfumo wa umeng'enyaji chakula kufanya kazi vizuri.

Miili yetu pia huitumia sodiamu kloridi kama chumvi kuufanya ubongo, uti wa mgongo, machozi, mifupa, tezi za jasho, ogani na damu kufunikwa na chumvi.

Mwili unanufaika pia kutoka katika madini mengine yaliyomo katika chumvi ili kuuweka katika hali ya ualikalini na afya.

Ni kama na vile kwa kunywa maji kuzidi kunaweza kumuua mtu (hyponatremia), vivyo hivyo kwa kutumia chumvi kuzidi, kunaweza sababisha; uvimbe, kuharisha na kifo.

Chumvi ya mezani husafishwa kwa kuondoa madini madini na hupitishwa katika joto la nyuzi joto 1093. Kwa hiyo uliyonayo sasa ni asilimia 40 ya sodiamu na asilimia 60 ya kloridi, na kisha kemikali kama vile 'aluminium silicate' huongezwa ili kuifanya isishikane na hivyo kubaki katika hali ya unga. Aluminium silicate ni sumu kali inayoharibu mfumo wetu wa fahamu. Inatajwa kuwa ni miongoni mwa sababu zinazosababisha ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).

Sodiamu iliyozidi inaweza kutokea kutokana na kula vyakula vingi vyenye viongezi (additives) vya sodiamu. Sodiamu siyo chumvi, chumvi ni sodiamu-kloridi. Sodiamu bikaboneti, sodiamu benzoeti na monosodiamu glutameti (msg) ni baadhi ya viongezi hivyo.

Sodiamu, potasiamu na kloridi ni elektrolaiti (madini maalumu) ambayo huyeyuka katika maji na kubeba chaji za kiumeme na kuzipeleka sehemu zozote za mwili kuliko na maji. Madini haya yenye chaji za kiumeme yana uwezo wa kuingia na kutoka ndani ya seli kwa uhuru wote, huku yakipeleka lishe ndani na kubeba nje taka na maji yaliyozidi ili kuiacha seli katika hali yake ya usawa (balanced cell).

Wakati huo huo, kadiri elektrolaiti hizi zikitembea ndani na nje ya seli na kufanya mabadiliko yake, usawa maalumu wa Potasiamu ndani ya seli lazima utunzwe kwa kiasi maalumu cha sodiamu na kloridi ili kuishikilia potasiamu ndani katikati ya seli.

Elektrolaiti zinapatikana kwenye majimaji yote mwilini na hubeba mapigo (impulses) kwenye neva zetu. Kitendo hiki huusaidia moyo na kiwambo cha moyo (diaphragm) kusinyaa na kulegea.

Elektrolaiti hubeba Glukozi (damu yenye sukari) na kuipeleka ndani ya seli baada ya Insulini kufungua milango kwa ajili ya sukari kuchukuliwa.

Elektrolaiti pia huwasha pampu za kuzarishia nguvu ziitwazo kwa kitaalamu 'Cation pumps' ambazo huzarisha umeme ambao huifadhiwa kwenye beteri zijulikanazo kwa kitaalamu kama 'mg Adenosine Triphosphate (mgATP)' na 'mg Guanosine Triphosphate (mgGTP)' za mwili.

Ikiwa mtu atapungukiwa kwa kiasi kingi cha Elektrolaiti hizi kutokana na kuharisha au kwa sababu ya dawa za kukojosha (diuretics), anaweza kuwa mgonjwa sana na itamlazimu kwenda hospitali kupewa elektrolaiti hizi katika mfumo wa dripu (intraveneous fluid, IV), kama vile; maji chumvi (saline solution), maji sukari (dextrose fluid) na madini.

Siku hizi vinywaji vyetu vingi baridi vinaongezwa kafeina ambayo ni kikojoshi kinachoyalazimisha maji kutoka ndani ya mwili na kutusababishia upungufu wa maji mwilini (dehydration).

Kwa mjibu wa dr.Batmanghelidj, hakuna kinywaji ambacho ni mubadala wa maji.

Wanasayansi na madaktari bado hawaelewi ni kwa jinsi gani chumvi huyeyuka ndani ya maji au ni kwa vipi iwezavyo kuendelea kuwa na hali ya uchumvi na uchumvi. Wanasayansi na wanakemia wana baadhi za nadharia, lakini bado hawajaweza kuzithibitisha. Bado imebaki kuwa ni fumbo (mystery).

BAADHI YA KAZI ZINGINE MHIMU ZA CHUMVI MWILINI:


 • Chumvi huyalazimisha baadhi ya maji kubaki nje ya seli. Inarekebisha uwiano sawa wa kiasi cha maji yaliyopo nje ya seli. kuna bahari mbili za maji ndani ya mwili, bahari moja imejishikiza NDANI ya seli, na bahari nyingine ya pili imejishikiza NJE ya seli. Afya bora inategemea uwiano mzuri wa ujazo wa maji uliopo baina ya bahari hizi mbili, na usawa huu unawezeshwa pekee na chumvi, chumvi ambayo haijasafishwa (unrefined sea salt) ndiyo nzuri zaidi.

 • Chumvi husaidia kuondoa dalili za mfadhaiko (stress).

 • Figo hazitaweza kufanya kazi zake vizuri bila chumvi.

 • Kukata tamaa na matatizo ya kisaikolojia, vitaondolewa kwa kuchukuwa chumvi zaidi, kula mlo kamili na kufanya mazoezi ya kutembea.

 • Mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida yanaweza kurudishwa katika hali yake ya kawaida kwa kuchukuwa kipande cha chumvi na kukiweka mwishoni mwa ulimi na kukifanya kiyeyuke.

 • Mifupa inapata uimara wake toka katika chumvi, na siyo katika kalisiamu pekee.

 • Je wewe ni mwanaume na unashindwa kuhimili kusimama? unahitaji chumvi zaidi na kunywa maji halisi zaidi.

 • Kuichukuwa chumvi na kunywa maji kabla ya mazoezi, kutakusaidia kupumua vizuri na kutokwa na jasho chache.

 • Matatizo ya kibofu cha mkojo na upotevu wa mkojo wa makusudi, vingeweza kurekebishwa kwa kuongeza chumvi zaidi kwenye mlo wako.

 • Dalili za maumivu ya jongo (Gout) zinaweza kuzuiwa kwa kutumia chumvi.

 • Chumvi ni mhimu ili kuzuia kuvimba kwa mishipa na vena kwenye miguu.

 • Kwa sababu tunapata potasiamu karibu katika kila chakula tunachokula, chumvi inatakiwa kuongezwa katika milo yetu, hii itairuhusu miili yetu kuhimili usawa sahihi wa maji kati ya bahari ya ndani na ile ya nje ya seli.

 • Chumvi ni mhimu ili kuondoa asidi iliyozidi kwenye seli, hasa seli za ubongo.

 • Chumvi ni mhimu kwa ajili ya kusawazisha kiasi cha sukari kwenye damu, hivyo kuzuia ugonjwa wa kisukari.

 • Chumvi ni mhimu katika uzarishaji wa nguvu umeme itokanayo na maji katika seli zote za mwili.

 • Chumvi ni mhimu katika mawasiliano ya neva na ufanikishwaji wa taarifa wakati wote seli za ubongo zinapofanya kazi tangu kuzaliwa hadi kufa.

 • Chumvi ni mhimu katika umeng'enywaji wa chakula na madini kwenye utumbo mdogo (intestinal tract).

 • Chumvi ni mdhibiti madhubuti dhidi ya histamini.

 • Chumvi ni mhimu ili kuzuia mikakamao ya mishipa (cramps).

 • Chumvi ni mhimu katika kusafisha makohozi na kubana kwa kifua.

 • Chumvi ni mhimu ili kuzuia uzarishaji wa kuzidi wa mate katika kiwango kwamba yanatoka nje ya mdomo wakati umelala, kitendo hiki cha kutoa mate (udenda) wakati umelala ni dalili ya upungufu wa chumvi mwilini.

 • Chumvi ina umhimu mubwa katika uimarishaji wa mifupa. Ugonjwa wa mifupa (osteoporosis) kwa sehemu kubwa, ni matokeo ya upungufu wa chumvi na maji mwilini.

 • Chumvi ni mhimu katika usafishaji wa makohozi mapafuni na maji yaliyogandamana hasa kwa watu wenye pumu, ikiwa inakulazimu kusafisha koo kila wakati, ni dalili kuwa umepungukiwa chumvi.


CHUMVI KIASI GANI:
Dr.Batmanghelidj anashauri; ¾ (robotatu) gramu za chumvi kwa kila nusu lita ya maji (16 ounces), au nusu kijiko cha chakula kwa kila nusu galoni ya maji, au kijiko kimoja cha chakula kwa kila galoni moja la maji tunayokunywa. Hiki ni kiasi kizuri kwa kuanzia na siyo kanuni, tafadhari tumia aina ya kijiko kilichotajwa hapo juu kwa vipimo sahihi.

Ukiona viwiko, vidole au kope za macho zinavimba, usitumie chumvi kwa siku 2, kunywa maji halisi pekee na kisha siku ya tatu, endelea kuchukuwa chumvi tena.NAMNA ZA KULA CHUMVI:


 • Njia ya kwanza ni kuiweka chumvi katika sehemu ya mbele ya ulimi, hakikisha unaihisi radha yake, na kisha kunywa maji juu yake yakiisafisha kuelekea chini.

 • Unaweza pia kuongeza chumvi ya ziada kwenye chakula chako.Tatizo la njia hii ni kuwa, chakula kinahisika kuwa na chumvi zaidi ya radha zingine.
  kuichanganya chumvi pamoja na maji ya kunywa si wazo zuri sana.
Source: maajabuyamaji2.artisteer.net/chumvi 


News Alert: Marumbano ITV: Wachina kufanya kazi ambazo watanzania wa kawaida wanaweza kuzifanya inasaidia kuleta

Wachangiaji waliowengi wamekataa kuwa si maendeleo. Nimependa sana wageni wa leo.
Wamejitahidi kuonesha usomi wao ila kuna kijana mmoja anasema kuna benki ya vijana na
akajibiwa kuwa hiyo ni ya CCM (UVCCM) na kuwa atakuwa na asilimia sifuri.
 Click here to safely unsubscribe from "JamiiForums | The Home of Great Thinkers." Click here to view mailing archives, here to change your preferences, or here to subscribe


Your requested content delivery powered by FeedBlitz, LLC, 9 Thoreau Way, Sudbury, MA 01776, USA. +1.978.776.9498